Thursday, March 12, 2020

NAHODHA WA REAL MADRID AWATAKA WACHEZAJI KUJIKOSOA ILI KUTWAA UBINGWA WA LALIGA


SERGIO Ramos, nahodha wa timu ya Real Madrid amesema kuwa wana kazi ngumu ya kufanya ili kufikia malengo waliyojiwekea ya kutwaa ubingwa wa La Liga .

Real Madrid ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Betis jambo lililowaumiza wachezaji wengi ndani ya kikosi hicho.

Ramos amesema kuwa bado nafasi ya kutwaa ubingwa ipo lakini haitatimia iwapo watashindwa kujikosoa pale walipokosea ili wawe bora zaidi. 


"Tunapaswa tujikosoe wenyewe na kuona namna gani tutakuwa bora, ili tutwae ubingwa ni lazima kuboresha utendaji wetu wa kazi na kutimiza majukumu yetu kwa bidii," amesema.

Madrid ipo nafasi ya pili na ina pointi 56 imecheza mechi 27 sawa na Barcelona ambao ni vinara wana pointi 58

Friday, March 6, 2020

Arsenal yaishia 32 bora Europa League

Club ya Arsenal ya England imeondolewa katika michuano ya Europa League kwa kufungwa 2-1 nyumbani kwao dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki katika uwanja wa Emirates game hiyo ikienda dakika 120.
Hivyo baada ya Olympiacos upata goli la ushindi dakika ya 120, ikafanya mchezo umalizike 2-1 na matokeo ya jumla (aggregate) ikawa 2-2, Arsenal akaondolewa katika michuano hiyo kwa kuruhusu kufungwa magoli mengi nyumbani

iverpool yapata pigo Allison Becker kuwakoss Bournemouth na Atletico

Club ya Liverpool ya England ikiwa ina machungu ya kipigo cha kwanza EPL dhidi ya Watford kesho itakuwa nyumbani katika mchezo wa EPL kuikabili FC Bournemouth, lakini Liverpool wataingia wakiwa na wakati mgumu katika mchezo huo kwa sababu imethibitika kuwa wanamkosa golikipa wao namba 1 Allison Becker kutokana na kupata majeraha.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha taarifa hizo jioni ya leo na kuongezea kuwa Becker ataukosa pia mchezo muhimu wa marudiano wa hatua ya 16 bora wa UEFA Champions League dhidi ya Atletico Madrid ambao wanahitaji kupindua matokeo na kutetea Ubingwa wao kutokana na mchezo wa kwanza ugenini Liverpool alifungwa 1-0.

MECHI TANO ZA MWISHO, ZINAIAMUA DABI YA KARIAKOO NAMNA HII




Na Saleh Ally
GUMZO la Dabi ya Kariakoo limerejea tena, kila mmoja anajua anachokiamini na anazungumza anachoona ndio sahihi.

Nani atashinda? Ni suala lenye maswali mengi ambayo kawaida huwa hakuna uhakika wa majibu lakini takwimu zinaweza kuwa na nafasi ya kwanza kutengeneza njia ya kuangalia mchezo ukoje.

Kikubwa mchezo wa Dabi, hasa hii ya Kariakoo huwa unashangaza kwa kuwa wakati mwingine hata takwimu nazo zinapigwa bao kutokana na ugumu wenyewe wa mchezo.

Pamoja na kwamba takwimu za nyuma wakati mwingine zinashindwa kuweka wazi mwendo wa Dabi ya Kariakoo inavyokuwa, lakini hauwezi kuzikwepa wakati unapozungumzia ujio wa mchezo huo.

Angalia mechi tano zilizopita za Yanga ambao watakuwa wenyeji lakini mechi tano za Simba watakaokuwa wageni utagundua kuna jambo na linaweza likawa linaashiria kuwa hautakuwa mchezo laini.

Nasema hautakuwa mchezo laini kwa maana ya kupata matokeo kwa wepesi ingawa kweli, inawezekana kuwa na matokeo ya kushangaza.

SIMBA:
Takwimu za mechi 5 zilizopita kwa upande wa wageni Simba zinaonyesha hivi; wameshinda zote 5 na kukusanya pointi 15.

Katika mechi hizo tano, Simba wamefunga mabao 10 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara tatu tu.

Kama utafanya tathmini za karibu katika mechi tatu za mwisho, Simba pamoja na kufunga mabao mengi, nyavu zake zimeguswa zaidi ya Yanga.

Katika mechi hizo tatu, Simba imefunga mabao nane na kuruhusu matatu. 


YANGA:
Kwa upande wa Yanga, katika mechi zao tano wameshinda mbili tu wakitoa sare mechi tatu na kukusanya pointi tisa. 

Yanga wamefunga mabao matano na kuruhusu bao moja tu la kufungwa.

Ukifanya tathmini ya mechi tatu za mwisho, Yanga imefunga mabao manne na haikufungwa hata bao moja. Ilikutana na Coastal ikawa sare ya 0-0, mechi mbili za mwisho ikashinda 2-0 kila mechi dhidi ya Alliance na Mbao.

Kipimo cha mwisho unaona Yanga ina safu bora ya ulinzi katika mechi hizi tatu na baadaye tano za mwisho kutokana na kuruhusu mabao machache ya kufunga.

Safu ya ulinzi ya Kelvin Yondani na Lamine Moro pamoja na Jaffary Mohammed na Juma Abdul iko vizuri zaidi katika kutoruhusu mabao.

Kazi ya safu ya ulinzi ya Luc Eymael imeimarika zaidi na ngumu kufungika lakini inakutana na safu kali zaidi ya ushambulizi katika Ligi Kuu Bara.

Safu ya Meddie Kagere, Luis Miquissone, Cletous Chama na John Bocco ni hatari zaidi na unaona namna wanavyokwenda wakiwa wamefunga mabao 55 katika mechi 26 na Yanga katika mechi 24, wao wamefunga mabao 29.

Ukisema uangalie kwa ujumla, kidogo inaweza ikakupoteza zaidi kwa kuwa safu ya Simba inaonekana ni ngumu zaidi kwa kufungwa mabao 14 tu na Yanga kuruhusu mara 18.

Ndio maana nikasisitiza, vizuri kuangalia katika hizo mechi tano au tatu zilizopita kwa kuwa zinaonyesha kazi ya makocha wote akiwemo Eymael ambaye hata mechi ya kwanza ya Dabi ya Kariakoo, hakuwa ameanza kazi Yanga.

Katika soka kama nilivyoeleza awali, takwimu ni nzuri kutengeneza mwelekeo kwa maana ya mwendo wa mechi inayofuata lakini bado haziwezi kuwa mwamuzi wa kila kitu.



MECHI 5 ZA SIMBA LIGI KUU
Lipuli 0-1 Simba Samora
Simba 1-0 Kagera Taifa
Simba 3-1 Biashara         Taifa
Simba 2-0 KMC Taifa
Azam 2-3 Simba Taifa



MECHI 5 ZA YANGA LIGI KUU
Yanga 0-0 Prisons Taifa
Polisi     1-1 Yanga Ushirika
Coastal  0-0 Yanga Mkwakwani
Yanga 2-0 Alliance         Taifa

Yanga 2-0 Mbao Taifa

AHADI ZA FEDHA KWA WACHEZAJI YANGA VS SIMBA NI KUONYESHA TUMEPITWA NA WAKATI




NA SALEH ALLY
WAPENDA soka lazima watakwenda Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakiwa na mambo mengi kichwani tayari kuishuhudia mechi ya watani wa jadi Yanga watakaokuwa wenyeji wakiwakaribisha Simba keshokutwa Jumapili.

Bila shaka itakuwa mechi nyingine ambayo inajitegemea kama ambavyo zimekuwa mechi nyingi za watani wa jadi wanapokutana.

Haiwezi kufanana na mechi nyingine kwa kuwa kila mechi ya watani inakuwa na sababu zake za kupatikana au kufanyika.

Katika mechi ya keshokutwa, Yanga watakwenda uwanjani kikubwa zaidi wanakitaka ni heshima na kidogo kujaribu kuikamata Simba, jambo ambalo kiuhalisia linaweza kuwa na wepesi tu kama Simba watakuwa si makini katika mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Bara.

Ndio maana nikasema, Yanga watataka heshima lakini pili ni kuthibitisha kwamba ile sare ya mabao 2-2 baada ya tambo nyingi za Simba, kwao haikuwa ya kubahatisha.

Hayo ni mawazo ya tambo za soka lakini hebu tujadili kuhusiana na hizi ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa kila unapofikia mchezo wa watani wa jadi.

Umesikia wewe mwenyewe kuwa klabu moja imewaahidi wachezaji wake kiasi fulani cha fedha kama wakiifunga Yanga au Yanga wakiifunga Simba.

Viongozi wanalazimika kuweka dau mezani ili wachezaji wacheze vizuri na kuhakikisha wanapata ushindi, binafsi naona ni jambo la kufedhehesha mpira wenyewe na hili linatubakiza nyuma sana sisi katika mchezo wa soka.

Wachezaji wanaijua kazi yao, wanatambua wajibu wa kuifunga Simba au Yanga na wanajua umuhimu wa ushindi ndio maana hufanya mazoezi kwa juhudi kubwa, husikiliza maelekezo ya mwalimu kwa usikivu wa juu ili kuhakikisha wanafanikisha ushindi.

Juhudi zao pamoja na kujua watapata pointi tatu ambazo ni muhimu lakini wanajua namna inavyokuwa heshima kushinda dhidi ya mtani wao kwa kuwa mashabiki ambao huwaunga mkono wanahitaji ushindi huo kwa nguvu zote na lazima kuwafurahisha.

 Angalia, wakati unawafurahisha watu unaotegemea wakuunge mkono, wakati huohuo unapata pointi zako muhimu ambazo zinaifanya kazi yako kuwa imetukuka. Sasa kuna haja gani ya kuongezewa dau la fedha ili uifanye kazi yako kwa ufasaha?

Binafsi huwa sioni ni jambo sahihi na wakati mwingine tunapaswa kwenda na wakati na kujifunza kutengeneza wachezaji wanaojitambua kwa kuwaacha wafanye kazi yao kwa weledi na viongozi wafanye yao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawalipa fedha zao kwa maana ya posho na mishahara kwa wakati.

Tunaweza tukawa tunaona jambo hili ni dogo kwa kuwa tu ushabiki umewazidi wengi nguvu lakini hili jambo ni ugonjwa mkubwa sana ambao huenda tiba yake inaweza ikachukua muda mrefu sana kupatikana.


Wachezaji wanapaswa kulipwa vizuri na kupata kila kinachostahili ili wafanye vizuri. Wakati mwingine klabu zinalazimika kuwa watumwa kwa kuomba fedha kwa wafadhili ambao wakati mwingine nao wanakuwa na masharti yao baadaye, jambo ambalo si sawa.

Klabu zinalazimika kuwa watumwa kwa kuwa zinahitaji fedha za “kuwanunua” wachezaji wake ili waweze kuifanya kazi yao vizuri ya kumfunga mtani kwa kuwa kama watapoteza viongozi watakuwa katika wakati mgumu na hawaitaki hiyo presha.

Mikataba ya wachezaji na klabu haionyeshi hilo kwamba lazima wapewe fedha ndio wacheze vizuri dhidi ya Yanga au Simba. Kuendelea hivi ni kuendelea kutengeneza furaha ya kipindi hiki tu lakini uhalisia, tunatengeneza bomu kwa muda mrefu sana na kuna siku litakuwa tatizo kubwa ambalo kulimaliza kutahitaji nguvu nyingi sana.

 Mfano, klabu imeahidi Sh milioni 150 kwa wachezaji waifunge Yanga au Simba, kwa nini fedha hizo zisingetumika kutengeneza uwanja au kuwakuza vijana kwa kuwanunulia vifaa sahihi wachezaji wa vijana au ziwe mishahara au posho za wachezaji wa timu za vijana na wanawake kwa muda wa miezi mitatu, minne kuliko iishe siku moja kwa kuwalipa wale ambao walishalipwa kwa mujibu wa mkataba!


Nawakumbusha, tuliache hili kwa kuwa kuendelea kulifanya ni kufanya mambo ya leo tu bila ya kuangalia kesho ya mpira itakuwaje.

Thursday, March 5, 2020

Ighalo aitendea haki nafasi yake Man United

Club ya Man United usiku huu ilikuwa ugenini kucheza game yake ya 16 bora ya FA Cup dhidi ya Derby County ikiwa ndio mbio za kuwania kutinga robo fainali.
Mchezo huo wa Man United ulikuwa unawakutanisha na mchezaji wao wa zamani Wayne Rooney aliyeishia kuona timu yake ya Derby ikipoteza kwa magoli 3.0.
Hata hivyo baada ya Luke Shaw kufunga goli la uongozi dakika ya 33, Jude Ighalo ambaye anatajwa kama ingizo jipya akafunga magoli mawili dakika ya 41 na 70 na kuitendea haki nafasi hiyo ikiwa yupo hapo kwa mkopo, Man Unite sasa robo fainali watacheza dhid ya wababe wa Spurs club ya Norwich City

Mourinho azungumzia kitendo cha Eric Dier kumvaa shabiki

Kocha wa Tottenham Hotspurs Jose Mourinho amekemea kitendo cha mchezaji wake Eric Dier kuwa sio kizuri na wala sio cha kiuanamichezo.
Dier mara baada ya mchezo wa 16 bora wa FA Cup wa Spurs dhidi ya Norwich City uliyomalizika kwa Spurs kuondolewa kwa kufungwa kwa penati 3-2 Dier alienda kumvaa shabiki.
”Siwezi kulikimbia swali lako nafikiri Dier amefanya kitu ambacho proffesional hawezi kukifanya lakini kwa mazingira kama haya kila mmoja wetu angeweza kufanya”>>> Mourinho

MFAHAMU REFARII WA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA, ANA BALAA SIO KITOTO

JOTO limezidi kupanda kuelekea Machi 8 ambapo kutakuwa na mchezo kati ya Yanga na Simba uakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtaja Martin Saanya mwenye ngome yake Morogoro ambaye ana beji ya FIFA atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo dhidi ya Yanga na Simba utakaopigwa majira ya saa 11:00 jioni.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, mwamuzi msaidizi namba 1 atakuwa ni Mohamed Mkono (Tanga), mwamuzi msaidizi namba 2 ni Frank Komba wa Dar es Salaam na mwamuzi wa akiba atakuwa ni Elly Sasii kutoka Dar es Salaam.

Katika mchezo huo pia kutakuwa na waamuzi wasaidizi wa ziada ambao ni Abdallah Mwinyimkuu kutoka Singida na Ramadhani Kayoko wa Dar es Salaam, wakati mtathmini wa waamuzi akiwa ni Sudi Abdi wa Arusha na kamishna wa mchezo atakuwa Mohamed Mkweche wa Dar es Salaam.


Kocha Luc Eymael amewahi kumlalamikia mwamuzi Martin Saanya kuwa aliinyima Yanga penalti katika mechi dhidi ya Mbeya City. Eymael raia wa Ubelgiji alimlalamikia Saanya kutotoa penalti baada ya Bernard Morrison kuchezewa rafu na mlinzi wa Mbeya City katika mechi ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1.

 Kwa Simba wakati Jonas Mkude akitolewa kwa kadi nyekundu msimu wa mwaka 2016 kwenye sare ya kufungana bao 1-1 alikuwa kati hivyo wote wana historia naye

Mourinho hali tete atupwa nje ya FA Cup na Tottenham yake

Club ya Tottenham Hotspurs wameaga michuano ya FA Cup baada ya kuondolewa kwa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Norwich City kutokana na game hiyo kwenda dakika 120 kumalizika sare ya kufungana moja moja kama ilivyokuwa katika mchezo wa kwanza.
Jose Mourinho akiwa na kikosi chake cha Tottenham amekuwa na wakati mgumu kutokana na timu yake kuondolewa mapema, ushindi huo wa Norwich unamfanya acheze na mshindi wa mechi ya Derby County dhidi ya Man United.
Michezo ya robo fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kati ya March 20 na 22, timu zilizofu kucheza hatua ya robo fainali ni Man City, Leicester, Norwich, Arsenal, Sheffield United, Newcasle United na Chelsea

YANGA YAIPOYEZA SIMBA

ZIMEBAKI siku tatu kuwakutanisha  Yanga na Simba Uwanja wa Taifa kwenye mechi nne za hivi karibuni ambazo ni dakika 360 Yanga imeipoteza Simba kwa kucheza mechi hizo bila kuruhusu bao.
Safu ya Yanga ya ulinzi inayoongozwa na Lamine Moro pamoja na Juma Abdul imeonyesha ukomavu kwa kuipoteza ile ya Simba inayoongozwa na Pascal Wawa sambamba na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Yanga imecheza mfululizo bila kuruhusu bao ilikuwa ni Februari 23 mbele ya Coastal Union 0-0, Februari 26,Gwambina FC 0-1 huu ulikuwa ni wa FA, Februari 29 Alliance 0-2 na Machi 3, Yanga 2-0 Mbao FC. Simba ndani mechi zao nne ambazo wamecheza mfululizo kabla ya mechi ya jana dhidi ya Azam FC walifungwa mabao 2 kwenye ushindi wa mabao 3-1, Februari 22, dhidi ya Biashara United, Februari 25 waliruhusu bao kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Stand United kwenye sare ya kufungana bao 1-1, ila walishinda kwa penalti 3-2 na kutinga hatua ya robo fainali.
Februari 18 haikufungwa mbele ya Kagera Sugar ikishinda bao 1-0 na Machi Mosi haikufungwa na KMC wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kwenye mechi hizo nne mfululizo Yanga imefunga mabao matano bila kuruhusu bao na Simba imefungwa mabao mawili na kufunga mabao sita

Wednesday, March 4, 2020

AZAM FC YA SEMA KILICHO WAKWAMISHA TAIFA JUMLA MBELE YA SIMBA

AGREY Moriss, nahodha wa Azam FC amesema kuwa walishindwa kupata ushindi mbele ya Simba jana Uwanja wa Taifa kutokana na makosa yao wenyewe.

Kwenye mchezo uliochezwa Machi 4, Azam ilikubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Simba na kupeperusha pointi tatu muhimu.

"Tulianza kwa kasi na kushindwa kuzitumia nafasi ambazo tulizipata wapinzani wetu waliweza kutumia nafasi walizotengeneza wakatushinda na huu ndio mpira na haya ni matokoe, tunajipanga," amesema. 

Azam FC imepigwa nje ndani na Simba msimu kwa jumla ya mabao 4-2, mchezo wa kwanza walifungwa bao 1-0 na mchezo wa pili walifungwa mabao 3-2.

AZAM FC YA SEMA KILICHO WAKWAMISHA TAIFA JUMLA MBELE YA SIMBA

AGREY Moriss, nahodha wa Azam FC amesema kuwa walishindwa kupata ushindi mbele ya Simba jana Uwanja wa Taifa kutokana na makosa yao wenyewe.

Kwenye mchezo uliochezwa Machi 4, Azam ilikubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Simba na kupeperusha pointi tatu muhimu.

"Tulianza kwa kasi na kushindwa kuzitumia nafasi ambazo tulizipata wapinzani wetu waliweza kutumia nafasi walizotengeneza wakatushinda na huu ndio mpira na haya ni matokoe, tunajipanga," amesema. 

Azam FC imepigwa nje ndani na Simba msimu kwa jumla ya mabao 4-2, mchezo wa kwanza walifungwa bao 1-0 na mchezo wa pili walifungwa mabao 3-2.

HIZI APA 18 ZA KUTAFUTA POINT 3 UWANJANI


Leo Machi 4 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara mambo yanazidi kupamba moto ambapo timu 18 zitakuwa kazini kwenye viwanja tisa kuzisaka pointi tatu namna hii:- 

Azam FC v Simba, Taifa.

Singida United v Coastal Union, Namfua.

Mwadui FC v Polisi Tanzania, Kambarage.

Biashara United v Prisons, Karume.


Ruvu v Alliance, Mabatini.

Mtibwa v Namungo, Gairo.

Kagera Sugar v Mbeya City, Kaitaba.

Lipuli v Ndanda, Samora.

KMC v JKT Tanzania, Uhuru


Mechi zote zitachezwa saa 10:00 jioni isipokuwa ile ya Azam v Simba itakuwa saa 1:00 usiku, Uwanja wa Taifa

Victor Wanyama aondoka Tottenham, amfuata Thierry Henry

Nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya 'Harambee Stars' na kiungo wa Tottenham Hotspurs, Victor Wanyama, ameachana na klabu hiyo.

Wanyama alisajiliwa na Spurs kutokea Southampton mwaka 2016 na kufanikiwa kuichezea michezo 69, akifunga mabao sita na mafanikio makubwa aliyoyapata ni kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu nchini Uingereza pamoja na kikosi chake kufika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Wanyama ameandika ujumbe wa kuishukuru Spurs kwa kipindi chote cha miaka minne alichohudumu na kikosi hicho.


Amejiunga na klabu ya Montreal Impact inayoshiriki Ligi kuu ya nchini Marekani (MLS), chini ya mchezaji nguli wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry.

MBWANA SAMATTA AWEKA WAZI WANAESIMAMIA SHUGHULI ZAKE ZA KISOKA

NI Headlines za mchezaji Mbwana Samatta ambae time hii ameweka wazi juu ya uongozi unaosimamia shughuli zake, mchezaji huyo anayekipiga kwenye club ya Aston Villa kupitia ukurasa wake wa twitter aliwajulisha mashabiki na kuandika ‘Ningependa kuwataarifu Kuwa kampeni zote za matangazo na biashara zitakuwa zinafanyika chini ya Emmanuel Ale, Tafadhali piga/WhtsApp +255768259371’- Samatta 
Maamuzi hayo yamefanywa na mchezaji huyo baada ya hivi karibuni kuibuka kwa watu wasiojulikana wakidai wanamsimamia Mbwana Samatta huku wengine wakifunguka feki akaunti zenye jina la Samatta wakiomba misaada mitandaoni

SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KWA AZAM FC


UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kumalizana na Azam FC leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa majira ya saa 1:00 usiku.

Azam FC itamenyana na Simba ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wakiwa na kumbukumbu ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wa leo watapambana kufikia malengo yao.

"Kazi ni moja tu kuendelea kutafuta ushindi ambao utatupa pointi tatu, ushindani ni mkubwa nasi pia tunapambana kutafuta matokeo

HIZI HAPA ZILIZOMTUNGUA AISHI MANULA NA ZILIZOMKOSA


Timu ya Simba ikiwa imecheza mechi 25, Manula amekaa langoni kwenye mechi 18 huku mechi saba akikaa mlinda mlango namba mbili Beno Kakolanya.

Simba ikiwa imefungwa mabao 13 amefungwa mabao 8.
Ametoka na clean sheet 12 ambapo ilikuwa ni mbele ya Kagera Sugar 0-3 Simba, Biashara United 0-2 Simba,Simba 1-0 Azam FC,Singida United 0-1 Simba,Simba 4-0 Mbeya City,Simba 0-0 Prisons,Ruvu Shooting 0-3 Simba, KMC 0-2 Simba,Mtibwa Sugar 0-3 Simba, Lipuli 0-1 Simba na Simba 1-0 Kagera Sugar, Simba 2-0 KMC.

Ametunguliwa mbele ya Simba 3-1 JKT Tanzania, Simba 2-1 Mtibwa Sugar, Mwadui 1-0 Simba, Simba 0-1 JKT Tanzania, Simba 2-2 Yanga, Biashara Uited 1-3 Simba

LAMPARD ACHEKELEA UWEZO WA VIJANA WAKE UWANJANI BAADA YA KUIBAMIZA LIVERPOOL MABAO


FRANK Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa vijana wake wanaimarika kila siku jambo linalompa matumaini ya kuendelea kuwa bora kwenye mechi zao zijazo.

Chelsea iliibamiza mabao 2-0 jana Liverpool kwenye mchezo wa FA England uliochezwa Uwanja wa Stamford Bridge unaoipa nafasi ya kusonga hatua ya robo fainai jumlajumla.


Mabao ya Chelsea yaliyofungwa na Willian dakika 13 kipindi cha kwanza na Ross Barkley 64 kipindi cha pili.

Lampard amesema: "Ni kazi ngumu kuendelea kuwa bora lakini inawezekana iwapo wote tutakuwa na jambo moja la kufanya kwa kushirikiana, ninaona vijana wanazidi kuwa bora kila iitwapo leo,",

HIZI HAPA LEO 18 UWANJANI KUSAKA POINTI TATU


Leo Machi 4 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara mambo yanazidi kupamba moto ambapo timu 18 zitakuwa kazini kwenye viwanja tisa kuzisaka pointi tatu namna hii:- 

Azam FC v Simba, Taifa.

Singida United v Coastal Union, Namfua.

Mwadui FC v Polisi Tanzania, Kambarage.

Biashara United v Prisons, Karume.


Ruvu v Alliance, Mabatini.

Mtibwa v Namungo, Gairo.

Kagera Sugar v Mbeya City, Kaitaba.

Lipuli v Ndanda, Samora.

KMC v JKT Tanzania, Uhuru


Mechi zote zitachezwa saa 10:00 jioni isipokuwa ile ya Azam v Simba itakuwa saa 1:00 usiku, Uwanja wa Taifa